RAIS SAMIA ATANGAZA ONGEZEKO LA MSHAHARA KWA ASILIMIA 35.1 | PRESIDENT SAMIA ANNOUNCES 35.1% SALARY INCREASE

President Samia Suluhu Hassan has announced a 35.1% salary increase for public servants starting July 2025, aimed at improving the quality of life for
RAIS SAMIA ATANGAZA ONGEZEKO LA MSHAHARA KWA ASILIMIA 35.1 | PRESIDENT SAMIA ANNOUNCES 35.1% SALARY INCREASE
Rais Samia Atangaza Ongezeko la Mshahara kwa Asilimia 35.1 Mei 1, 2025 | Singida, Tanzania Katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) yaliyofanyika leo mkoani Singida , Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan , ametangaza habari njema kwa watumishi wa umma nchini. Katika hotuba yake, Rais Samia amewapongeza wafanyakazi kwa kujituma na kuunga mkono juhudi za serikali, hatua iliyosaidia uchumi wa taifa kukua kwa asilimia 5.5 mwaka huu . “Sasa kwa mapenzi makubwa na kwa namna mlivyoiunga mkono serikali tulipowaomba mfunge mkanda na mkaamua kujituma na kufanya kazi kwa bidii na mkafanya uchumi wetu ukue... Kwakuwa mcheza kwao hutunzwa,” alisema Rais Samia. Rais ametangaza kuwa kuanzia Julai 2025 , serikali itaongeza kima cha chini cha mshahara kwa watumishi wa umma kwa asilimia 35.1 . Kima cha chini kitaongezeka kutoka TSh 370,000 hadi TSh 500,000 , huku ngazi nyingine za mishahara zikipanda kulingana na bajeti ya serikali. Hatua hii ni ishar…